Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itafungua rasmi na kuanza kutumika Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lililojengwa katika eneo la Ndea Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Hata hivyo, sehemu anayoizungumzia Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo inatengenezwa sasa hivi na ni kweli mkandarasi yuko site hata jana nimepata uthibitisho huo ni kutoka pale kwenye lango mpaka kufika mpakani mwa Wilaya ya Mwanga na hifadhi. Sasa, kipo kipande cha kutoka pale kwenye mpaka kufika sehemu inaitwa Nadung’oro ambapo ndiyo ndani ya Kijiji cha Ndea ni kama kilometa nne, ilishatengenezwa lakini kwa sababu haijatumika muda mrefu ina maeneo korofi. Je, Serikali inatuambia nini juu ya ukamilishaji wa kipande hicho kutoka pale kwenye mpaka wa hifadhi mpaka kufika Nadung’oro ili wananchi wa Mwanga waweze kufika kwa urahisi kwenye lango hilo litakapofunguliwa? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kipande anachokizungumzia, kimsingi siyo kilometa nne tu ni kilometa 13.5 ambazo zinasimamiwa na wenzetu wa TARURA kwa upande wa Mwanga. Taarifa tulizonazo ni kwamba kipande kile kilifanyiwa kazi mwaka 2024, lakini kwa sababu barabara ile ilikuwa haitumiki imeota majani na haiwezi kutumika kiurahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, kwa sababu sisi tuna interest na eneo hilo ili kuweza kuingia kwenye hifadhi na kwa sababu Mheshimiwa Mbunge ameomba tuone jinsi ambavyo tunaweza kushughulikia kipande hicho, tumelichukua wazo lake tutawasiliana na wenzetu wa TARURA ili waweze kutupa kibali tuweze kukwangua na kusafisha eneo lile ili barabara iweze kupitika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved