Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Finance Wizara ya Fedha 183 2025-02-11

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuweka Kituo cha Forodha katika Kijiji cha Muhange, Nyabibuye na Malenga ili kuongeza kipato kupitia forodha mipakani?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha kuwa Serikali inatatua changamoto ya kukosekana kwa huduma za kiforodha katika Vijijiji vya Muhange, Nyabibuye na Malenga imepeleka Maafisa wa Forodha wawili eneo la Muhange kwa ajili ya huduma za forodha. Maafisa wanaohudumia Kituo cha Nyaronga wataanza kuhudumia Nyabibuye kwa awamu kabla ya kufungua ofisi ya huduma na eneo la Malenga litahudumiwa na maafisa kutoka Muhange.