Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuweka Kituo cha Forodha katika Kijiji cha Muhange, Nyabibuye na Malenga ili kuongeza kipato kupitia forodha mipakani?

Supplementary Question 1

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili modogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kukosekana kwa watumishi katika maeneo ya mpakani hasa katika mipaka ya Muhange, Nyabibuye na Malenga kunapelekea Serikali kupoteza fedha nyingi kwa sababu hazina wakusanyaji. Sasa, katika majibu yake ametaja watumishi wawili kwenda kuhudumia maeneo matatu tofauti ambayo yako mbali. Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi ili waweze kutosheleza kwa kila eneo ambalo nimelitaja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ili watumishi waweze kufanya kazi vizuri ni pamoja na uwepo wa ofisi, nyumba pamoja na huduma kama ya usafiri; je, ni lini sasa Serikali itajenga ofisi za forodha na nyumba za watumishi ikiwa ni pamoja na uwepo wa magari katika mipaka ya Muhange, Nyabibuye na Malenga? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, alilolisema ni kweli kwamba watumishi wawili watakuwa kidogo kwa maeneo matatu, lakini tumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni ametoa kibali cha watu zaidi ya 1,000 ambao wapo katika mchakato wa ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato huu wa ajira utakapokamilika tutapeleka vijana hao (watumishi) katika maeneo hayo matatu aliyoyataja wa kutosha kabisa ndani ya mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, ni kweli kwenye vituo hivyo hatuna ofisi, lakini ninatoa maelekezo kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania apeleke vijana wafanye survey mwaka ujao wa fedha tuanze kujenga walau kituo kimoja. (Makofi)