Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 185 2025-02-11

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza:-

Je, wananchi wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki kati ya mwaka 2022 hadi 2024?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022-2024 jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababishwa na pikipiki kwa mchanganuo ufuatao: madereva wa pikipiki waliopata ajali na kufariki ni 759; abiria waliopanda pikipiki na kupata ajali zilizosababisha vifo vyao ni 283; na wananchi waliokuwa wanatembea kwa miguu kandokando ya barabara au njiani, ama waliokuwa wanavuka barabara na kupata ajali ya kugongwa na pikipiki na kufariki dunia ni 71.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito kwa madereva wote wanaoendesha pikipiki kuzingatia sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoathiri wananchi wengi na kupunguza nguvu kazi katika Taifa letu, ahsante.