Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza:- Je, wananchi wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki kati ya mwaka 2022 hadi 2024?

Supplementary Question 1

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; idadi ya wananchi 1,113 ni kubwa sana, je, ni nini mkakati wa Serikali kuzuia ili vifo hivi ambavyo vinazuilika visitokee?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; baadhi ya waendesha bodaboda wamekuwa wakipakia abiria zaidi ya mmoja kwa jina maarufu la mshikaki na hivyo kusababisha wale ambao wamepanda katika bodaboda hizo inapotokea ajali inawezekana kama ni wanne au watano wote wanaweza wakapoteza maisha. Je, Serikali haioni umefika wakati wa kupiga marufuku upandaji wa mishikaki ili kunusuru wananchi? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, suala la ajali ni kweli linaumiza Watanzania wengi na kupunguza nguvu kazi. Ninatoa wito kwa Kamanda wa Usalama Barabarani kuzingatia kusimamia Sheria za Usalama Barabarani. Pia, madereva wote kuhakikisha kwamba wanasimamia Sheria za Usalama Barabarani na kuzifuata. Vilevile, abiria, watembea kwa miguu na wadau wote wanaotumia barabara wahakikishe kwamba wanasimamia Sheria za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali ambazo siyo za lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu abiria zaidi ya mmoja, ninamwelekeza Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani kusimamia sheria. Pili, wadau wote, watembea kwa miguu, abiria wote na Watanzania tusikubali kupanda pikipiki zaidi ya mtu mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kila mtu achukue hatua za tahadhari kwa sababu mnapokuwa zaidi ya mmoja inapotokea ajali mnafariki wote. Kwa hiyo, ninatoa wito kwa abiria wote, unapoona kuna abiria kwenye pikipiki, basi usipande na wewe. (Makofi)