Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 186 2025-02-11

Name

Aziza Sleyum Ally

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:-

Je, lini Serikali itarudisha Somo la Domestic Science katika Mtaala wa Elimu ya Shule za Msingi Nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, somo la sayansi kimu (domestic science) lilianzishwa baada ya mitaala kubadilishwa mwaka 1979 kufuatia Azimio la Musoma ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya siasa ni kilimo na elimu kwa wote. Somo hili la sayansi kimu liliboreshwa zaidi na maudhui yake kuingizwa katika somo jipya la stadi za kazi mwaka 1997.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ilikuwa ni pamoja na kupunguza wingi wa masomo kutoka masomo 13 hadi masomo saba kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mtaala ulioboreshwa mwaka 2023 maudhui yanayoshabihiana na somo la sayansi kimu yameboreshwa zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya jamii, kukua kwa sayansi na teknolojia pamoja na soko la ajira. Hivyo, maudhui hayo kwa ngazi ya elimu ya msingi yapo kwenye somo la sanaa na michezo, ambalo ni somo la lazima na linafundishwa kuanzia darasa la tatu hadi la sita. Aidha, kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kuna mkondo maalum unaofundishwa masuala ya chakula na lishe ambao umejikita kuendelea kujenga maarifa katika eneo hili. Ninakushukuru.