Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aziza Sleyum Ally

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itarudisha Somo la Domestic Science katika Mtaala wa Elimu ya Shule za Msingi Nchini?

Supplementary Question 1

MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; ninaomba nichukue nafasi hii kulipongeza sana Azimio la Musoma. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kama Azimio la Musoma lilikuwa ni zuri sana lenye kuelimisha, wanafunzi walikuwa na uwezo wa kujua kupika, usafi na hata kujishonea nguo zao wenyewe tofauti na sasa hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana nami tuanzishe shamba darasa kwa kuteua shule moja pale Tabora ili kuweka mtaala kama huu wa Azimio la Musoma ili kuwa mfano kwa shule nyingine ili vijana wetu warudi kule tulikotoka sisi?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Aziza Sleyum na nitajibu yote kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la masomo pamoja na mitaala ni suala ambalo ni dynamic siyo static kwa maana kwamba ni lazima kufanya maboresho na marekebisho mara kwa mara. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba maazimio yote au mitaala yote ni bora au mizuri kulingana na muda ambao mitaala hiyo imeweza kutumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ninamweleza katika mfumo wa sasa ambao tumefanya maboresho ya sera pamoja na mitaala inafanya elimu yetu ya lazima iwe ni ya miaka 10. Miaka sita shule za msingi na miaka minne katika shule za sekondari. Kwa hiyo, katika mfumo wetu huu wa sasa, wanafunzi wote watakaomaliza watapata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea. Katika, darasa la kwanza na la pili, watoto watajifunza hayo masuala ya kushona, kufuma pamoja na mitindo na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo la pili alilolizungumza kuhusu Tabora kwamba tutengeneze pilot, ninadhani baada ya maswali tunaweza tukakutana na Mheshimiwa Mbunge, tukaangalia hilo wazo lako na ushauri wako, ni namna gani tunaweza kutekeleza kwa wakati. Ninakushukuru sana.