Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 188 2025-02-11

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-

Je ni lini Serikali itaanzisha Mfuko Maalum wa Mikopo ya Elimu ya Juu (Revolving Fund) ili kuongeza idadi ya wanufaika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu inatolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu iliyoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa Kitanzania wenye uhitaji na wanaostahili kupata mikopo na ruzuku ili kumudu gharama za masomo ya elimu ya juu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa inatumia fedha zinazokusanywa kutoka kwa warejeshaji walionufaika kama Mfuko wa Mzunguko ili kuwezesha wanafunzi wenye uhitaji waweze kupata mikopo. Hata hivyo, Serikali ipo katika mpango wa kufanya mapitio ya kina (comprehensive review) ya Bodi ya Mikopo ili kuwezesha wahitimu walionufaika kurejesha mikopo yao kwa urahisi. Mapitio haya yakikamilika yataimarisha mifumo ya urejeshaji mikopo na kuifanya Bodi ya Mikopo kuwa stahimilivu katika kujiendesha na kuongeza mapato pamoja na kuongeza idadi ya wanufaika kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.