Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:- Je ni lini Serikali itaanzisha Mfuko Maalum wa Mikopo ya Elimu ya Juu (Revolving Fund) ili kuongeza idadi ya wanufaika?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni lini hii comprehensive review inayofanyika itakamilika na kuleta majawabu katika Bunge hili?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, ni kwa namna gani hii comprehensive review imezingatia uhitaji wa wanafunzi wote wanaonufaika na mikopo hii katika kuhakikisha kwamba wote wananufaika na wanapata mikopo? (Makofi)
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Husna Sekiboko, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, comprehensive review kwa upande wa Bodi ya Mikopo tumeshakamilisha mwezi huu wa Februari kwa ujumla wake na kwa sasa tunafanya mapitio ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la mapitio ni kwa sababu shughuli za TEA na Bodi ya Mikopo zilikuwa kama zinalingana au zinafanana. Tumeona ni vyema vilevile tufanye mapitio ya Mamlaka ya Elimu ili kuweza kubaini zile shughuli ambazo zinashabihiana kuweza kuona kama tunaweza tukaziunganisha zikafanyika kwa pamoja. Kwa hiyo, mapitio haya ya Bodi ya Mikopo pamoja na TEA yatasaidia kuwa na muundo na utaratibu mzuri wa kuendesha Mfuko wetu huu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, mapitio yote haya mawili yatakapokamilika sasa, kwa maana ya TEA na yale ya Bodi ya Mikopo, lengo kuu ni kubainisha vile vyanzo vya mapato. Tutakapobainisha vyanzo vya mapato, tafsiri yake ni kwamba, tutaongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato pamoja na urejeshaji wa ile mikopo ambayo imetolewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya hivyo, mapato yote yatakuwa yameongezeka. Tunaamini kabisa baada ya mapitio haya na kubaini vyanzo vya mapato na kuongezeka kwa vyanzo vya mapato yetu, tafsiri yake ni kwamba, tunaenda kuongeza wigo wa wale ambao watakuwa wananufaika na mikopo hii au watakaokuwa wanapata mikopo kwa kiasi kikubwa sana. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved