Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 189 2025-02-11

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

Je, lini Serikali itamaliza tatizo la laini za simu za TTCL kutumika zaidi kutapeli wananchi?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha tatizo la matumizi mabaya ya laini za simu, ikiwemo laini za TTCL, linamalizika. Hatua hizo ni pamoja na:-

(i) Usajili wa laini kwa alama za vidole. Mfumo wa usajili wa laini kwa alama za vidole umelenga kudhibiti laini za simu zinazotumika kwa udanganyifu kwa kuhakikisha kila laini inahusishwa moja kwa moja na mmiliki wake halali;

(ii) Kufuatilia na kufungia laini zinazotumika kwa uhalifu. Serikali kupitia TCRA imeweka mifumo ya kufuatilia matumizi ya laini za simu na kuzifungia zile zinazobainika kutumika kwa ulaghai;

(iii) Kutoa elimu kwa umma. Serikali na wadau mbalimbali wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu jinsi ya kutambua ujumbe wa kitapeli na kuripoti matukio hayo kupitia namba 15040; na

(iv) Ushirikiano na watoa huduma za mawasiliano. TTCL na watoa huduma wengine wanashirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa, laini zinazotumika kwa ulaghai zinadhibitiwa mara moja.