Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza tatizo la laini za simu za TTCL kutumika zaidi kutapeli wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na kwa kweli, niseme tu kwamba, Serikali imekuwa inajitahidi sana kwenye eneo hili. Swali la kwanza; sasa, concern yetu kubwa ilikuwa ni pamoja na kuzifungia line, kwa nini hao matapeli ambao wanatapeli wananchi kwa kutuma ujumbe mfupi “tuma, halafu jina litatokea fulani”, wasikamatwe na kushtakiwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni kwa nini mitandao mingine, kama Vodacom, Airtel, wamefanikiwa wao wenyewe kudhibiti hali hiyo? Kwa nini TTCL line zake ndiyo zinatumika zaidi kwenye utapeli wa aina hiyo? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napokea shukrani zako na kukiri kwamba, sisi kama Serikali, tunafanya kazi kubwa sana kuhakikisha utapeli mitandaoni unakwisha. Vilevile kukamatwa na kushtakiwa, tayari wenzetu wa TCRA wameweza kudhibiti kwa sehemu kubwa, wachache wameweza kufikishwa kwenye vyombo vya dola na sheria imeendelea kuchukua mkondo wake. Hatutangazi kwa sababu, zoezi linaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii kwa nini TTCL inatumika zaidi; Mheshimiwa Mbunge nadhani ni experience yako binafsi, lakini ni mitandao yote ya watoa huduma inatumika na laini nyingi tunazozikamata siyo za TTCL peke yake ila hata watoa huduma wengine. Laini hizo zinaendelea kudhibitiwa, hivyo ninakutoa hofu na kwa kuzingatia TTCL ni taasisi ya Serikali, iko moja kwa moja ndani ya Wizara, tutaendelea kuweka nguvu na TCRA tutahakikisha tatizo hili la utapeli, kama tulivyoongea wiki iliyopita, Mheshimiwa Waziri Jerry Silaa alisimama hapa, tutaendelea kulishughulikia kuhakikisha linakoma kabisa, ahsante. (Makofi)