Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 190 2025-02-11

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Barabara ya Omugakorongo – Kigarama hadi Murongo utaanza baada ya kutangazwa upya?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, zabuni ya ujenzi wa Barabara ya Omugakorongo – Kigarama – Murongo (kilometa 110); Sehemu ya Murongo hadi Businde kilometa 53.4 imetangazwa upya baada ya zabuni ya awali kukosa Wakandarasi wenye sifa. Zabuni mpya ilitangazwa tarehe 6 Oktoba, 2024 na kufunguliwa tarehe 12 Desemba, 2024. Kwa sasa kazi ya uchambuzi wa zabuni inaendelea na inatarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Februari, mwaka huu wa 2025 na baadaye hatua za kumkabidhi mkandarasi zitaendelea. Ahsante.