Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Omugakorongo – Kigarama hadi Murongo utaanza baada ya kutangazwa upya?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; mlisema Barabara hiyo ya Omugakorongo – Kigarama – Murongo inajengwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza umesema imeshatangazwa, awamu ya pili ambayo inatoka Omugakorongo – Businde itatangazwa lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Barabara ya Omurushaka – Nkwenda – Murongo, mkandarasi alishalipwa tangu mwezi Septemba na alikabidhiwa ile barabara, lakini mpaka sasa hivi bado hajaanza, hatujamwona site. Shida iliyosababisha asianze kazi hiyo ni nini?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza, ni kweli kwamba, Barabara ya Murongo – Omugakorongo ndiyo barabara kuu ambayo inaunganisha Tanzania na Uganda kupitia Kyerwa. Tayari tumeshatangaza kipande cha kwanza ambacho tuko kwenye hatua za mwisho za manunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipande cha pili, tumeshakamilisha usanifu na tunaendelea kutafuta fedha ili tuweze kukamilisha kilometa zote 110 tukiamini kwamba, baada ya kukamilisha, basi upande huo tutakuwa tumekamilisha trunk road kama ilivyo sera yetu ya kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara zinazounganisha nchi na nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara aliyoitaja ya pili, ya Omurushaka – Nkwenda. Tayari tumeshamlipa mkandarasi na taarifa nilizonazo ni kwamba, mkandarasi yuko kwenye hatua za maandalizi ya awali, kwa maana ya mobilization. Kama kutakuwa na changamoto ya kuchelewa kwa sababu, tulishamlipa basi, Mheshimiwa Mbunge, tuweze kuonana naye, ili tuhakikishe kwamba, tunamsimamia. Ameshalipwa, aweze kwenda site na kuanza kazi. Ahsante.