Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 191 2025-02-11

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-

Je, ni hatua ipi imefikiwa na Serikali kuanza ujenzi wa Daraja la Kisorya – Lugezi linalounganisha Wilaya ya Ukerewe na Bunda?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kwa ajili ya Daraja la Kisorya – Lugezi na Barabara unganishi ya Nansio – Rugezi yenye urefu wa kilometa 11. Ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara unganishi kutoka Nansio hadi Rugezi, yenye urefu wa kilometa saba umeanza mwezi Februari, 2024. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja. Ahsante.