Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 192 2025-02-11

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanzisha Mfuko wa kuimarisha bei za mazao, ili kusaidia wakulima wa pamba na mazao mengine bei inaposhuka?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa kilimo imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo kupitia Tangazo la Serikali, Na. 22 la Tarehe 20 Januari, 2023, baada ya kuidhinishwa na Waziri wa Fedha. Mfuko huo umelenga kuchochea ukuaji wa maendeleo ya Sekta ya Mazao ya Kilimo, kupunguza ukali wa bei ya mazao inaposhuka, kutoa ruzuku ya pembejeo za kilimo (mbegu bora, mbolea pamoja na viuatilifu), kuchochea uwekezaji katika shughuli za utafiti wa kilimo na kuwajengea uwezo wakulima, wasindikaji, Maafisa Ugani na watafiti wa kilimo. Ahsante sana.