Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 193 2025-02-11

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Chela, Halmashauri ya Msalala?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Chela ina skimu ndogo ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 100 ambayo chanzo chake cha maji ni chemchemi ya asili. Kutokana na mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la watu, mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala iligharamia upembuzi yakinifu na usanifu wa awali, kwa ajili ya ujenzi wa bwawa na skimu ya umwagiliaji ya ukubwa wa hekta 700.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Halmashauri ya Msalala ipo kwenye mipango ya kutafuta fedha za kuwafidia wananchi wa maeneo ambayo bwawa hilo litajengwa. Aidha, skimu ya umwagiliaji katika Kata ya Chela imewekwa katika mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026, kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi na usanifu wa kina, ahsante.