Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Chela, Halmashauri ya Msalala?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri, lakini pia, ninaishukuru kwa ujenzi wa Skimu ya Mtambo ambao unaendelea. Swali langu la kwanza; Serikali iliahidi kufanya upembuzi yakinifu kwenye bajeti iliyopita katika Skimu ya Metrom, Longoi, Makeresho, Bwawa la Borutu, Skimu ya Ismail na Kikafu Chini. Je, ni lini sasa upembuzi yakinifu utafanyika kwenye skimu hizi, ili ujenzi uanze?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tuna mifereji ambayo ni muhimu sana kwenye kilimo cha Wilaya ya Hai. Ni lini sasa Serikali itaanza kujenga mifereji hii ifuatayo, muhimu sana, kwenye Wilaya ya Hai; Mfereji wa Bwana Mganga, Toweru, Shombole, Sonu, Maseti, Mriri, Indindi, Mwasha, Mpendaroho, Isawero, Johari na Magadini Kati?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Hai kwa kazi nzuri anayoifanya katika jimbo lake na kuwatetea wananchi, lakini namhakikishia tu kwamba, hizi skimu alizozitaja, Skimu ya Metrom, Longai, Makeresho, Kikafu Chini, zote tunaziingiza katika Mpango wa mwaka wa fedha 2025/2026, ili ziweze kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kwa ajili ya kupata gharama halisi tutafute mkandarasi na zianze kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, waambie wananchi wa Hai watakavyoendelea kukuchagua kuwa Mbunge, maana yake ni wawe na uhakika kwamba, skimu hizi zitakamilika kwa wakati, lakini vilevile, mifereji ambayo ameiainisha, tulishaipa kazi Tume ya Umwagiliaji kuifanyia vilevile upembuzi yakinifu, ili kupata gharama halisi tuweze kuwasaidia wananchi kwa kuijenga, waweze kutoa huduma kwa wakulima wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hayo ndiyo majibu ya msingi ambayo sisi Serikali tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge wa Hai, ahsante.