Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 274 2025-05-12

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha Watu wenye Ulemavu wanajikwamua kimaisha?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuwawezesha watu wenye ulemavu kujikwamua kimaisha, Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango, programu na miradi mbalimbali kwa kuzingatia sera na sheria zinazohusu masuala ya watu wenye ulemavu kama ifuatavyo:-
(i) Programu ya Ukuzaji Ujuzi iliyoanza kutekelezwa mwaka 2016;

(ii) Mikopo ya 10% isiyokuwa na riba inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo watu wenye ulemavu wametengewa asilimia mbili.

(iii) Utekelezaji wa takwa la Sheria ya Watu Wenye Ulemavu, Sura 183 la kutenga asilimia ya ajira kwa waajiri wenye watumishi kuanzia 20 na kuendelea kwa ajili ya waombaji wenye ulemavu.

(iv) Utekelezaji wa takwa la Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410 la kutenga 30% ya zabuni za umma kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu;

(v) Utekelezaji wa Mkakati wa Teknolojia Saidizi wa Mwaka 2024 - 2027;

(vi) Utekelezaji na Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ulemavu (Albinism) wa Mwaka 2024 – 2029; na

(vii) Utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali na ile ya kibajeti kama vile Mwongozo wa Teknolojia Saidizi.