Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 275 2025-05-12

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. FATMA HASSAN TAUFIQ K.n.y. MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wafanyakazi wa Majumbani unaozidi kukithiri kwenye Jamii?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi, lililoulizwa na Mheshimiwa Taufiq. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kulinda haki za wafanyakazi wote nchini wakiwemo wafanyakazi wa nyumbani. Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuridhia Mkataba wa ILO (International Labor Organization), Na. 189 kuhusu Kazi za Staha kwa Wafanyakazi wa Majumbani. Baada ya hatua hiyo kukamilika Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa kanuni mahususi kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Sura 366 ambayo imeweka katazo kuhusu unyanyasaji wa aina zote katika maeneo yote ya kazi. Ahsante.