Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 276 2025-05-12

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka magari ya wagonjwa katika Vituo vya Afya Iramba Ndogo na Mwasengela - Meatu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya za dharura na rufaa kwa kununua magari ya wagonjwa na kuyapeleka katika vituo vya huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024, halmashauri ya Wilaya ya Meatu imepokea magari matatu ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Meatu, ambapo magari mawili ya kubebea wagonjwa ya Kituo cha Afya Iramba Ndogo na Kituo cha Afya Mwasengela yameachwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu kwa muda na pindi majengo ya kutolea huduma za upasuaji wa dharura yatakapokamilika magari hayo yatapelekwa kwenye vituo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini.