Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka magari ya wagonjwa katika Vituo vya Afya Iramba Ndogo na Mwasengela - Meatu?

Supplementary Question 1

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kupata nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza ninapenda kuishukuru Serikali kwa kupeleka magari hayo katika hivyo vituo vya afya vya Wilaya ya Meatu, lakini magari hayo kweli hayajapelekwa. Kama alivyojibu Waziri kwamba mpaka wamalize miundombinu ya upasuaji ndiyo magari hayo yapelekwe. Swali la kwanza; kuna wagonjwa wengine wanaohangaika katika vituo hivyo vya afya na magari ni tatizo sana. Je, ni lini sasa Serikali itasema magari hayo yapelekwe kule? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; sambamba na hilo kuna upungufu mkubwa sana wa watumishi hasa madaktari katika hivyo Vituo vya Afya Mwasengela na Iramba Ndogo. Hakuna kabisa watumishi wa afya. Ni wawili tu walioko katika hivyo vituo vya afya na vituo hivyo, kwa mfano Iramba Ndogo ina wakazi 72,000 na Mwasengela inahudumia kata sita ambazo zina watu 62,000 na bado madaktari ni tatizo. Je, ni lini Serikali itapeleka hao wauguzi na madaktari?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Minza Mjika kwa maswali yake mawili ambayo yanalenga kuhakikisha kwamba huduma za afya zinaimarika na hasa katika mkoa na jimbo analotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la kwanza, kama nilivyojibu kwenye majibu ya msingi kwamba, magari haya matatu ya kubebea wagonjwa tayari yameshafikishwa katika Wilaya ya Meatu na ni suala la muda tu pale vituo hivi vya afya vitakapokuwa vimekamilika na vimeanza kutoa huduma za rufaa, basi magari haya yatapelekwa kwenye vituo hivyo vya afya kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusiana na watumishi, katika kazi mojawapo kubwa sana ambayo inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha sekta ya afya na hasa afya msingi inaimarika ni pamoja na kuajiri watumishi na kuwapanga katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya ili huduma bora za afya ziweze kupatikana. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Minza sauti yake Serikali imesikia na katika hizi ajira mpya za watumishi wa kada ya afya ninaomba nimhakikishie kwamba tutaweka kipaumbele katika kupanga watumishi wa kada ya afya katika vituo hivi vya afya vya Iramba Ndogo pamoja na Mwasengela. (Makofi)