Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 22 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 277 | 2025-05-12 |
Name
Robert Chacha Maboto
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda Mjini
Primary Question
MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Bunda imeanza ujenzi wa hospitali ya halmashauri mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo Serikali ilipeleka shilingi milioni 500 ambazo zimetumika kujenga jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la maabara. Aidha, jengo la wagonjwa wa nje limekamilika na linatoa huduma na jengo la maabara lipo hatua ya ukamilishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2022/2022 hadi 2024/2025, Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.45 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi lenye huduma za upasuaji wa dharura, jengo la upasuaji wagonjwa wa kawaida, wodi mbili za upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti na jengo la kufulia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa jengo la kuhifadhia dawa, jengo la mionzi pamoja na kukamilisha ujenzi wa majengo ya awali katika hospitali ya Mji Bunda.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved