Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 22 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 279 | 2025-05-12 |
Name
Toufiq Salim Turky
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:-
Je, kuna mpango gani kutatua changamoto za NEMC hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoathiri utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi. Ili kukabiliana na changamoto hizi hususani changamoto za kibajeti, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo:-
Kufanya mapitio ya Kanuni za Ada na Tozo za mwaka 2021 na kuongeza vyanzo vipya vya mapato na viwango vya tozo kwa miradi mikubwa ambayo shughuli zake zina athari kubwa kwenye mazingira; Kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa matumizi ya Kanuni mpya ya Ada na Tozo ya Mwaka 2024; Kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato (online billing system) ambayo inarahisisha ukusanyaji wa ada kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Baraza; na Kuboresha kanzidata ya miradi yote inayotakiwa kulipa ada na tozo za Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kukamilisha mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka ili kuipa nguvu ya kisheria (Legal Mandate) ya kusimamia majukumu yake ipasavyo na hivyo kujiwezesha kimapato; kufanya kaguzi za kimazingira katika miradi mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu na kuhimiza ulipaji wa ada na tozo za mazingira; na kuongeza idadi ya watumishi na kuanzisha Ofisi za Kanda ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuwafikia wadau wengi kwa muda mfupi katika maeneo mbalimbali nchini. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved