Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, kuna mpango gani kutatua changamoto za NEMC hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili. Swali la kwanza; je, ni lini sasa mchakato wa NEMC kuwa NEMA utakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, Serikali haioni haja ya kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa vyeti vya tathmini na ukaguzi kutoka NEMC? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Toufiq, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaanza mchakato wa kutoa NEMC kuipeleka kwenye NEMA; hii ni kwa sababu tumeona kweli kuna baadhi ya mapungufu ambayo sisi kama NEMC tunatakiwa tuyarekebishe. Kama nilivyoeleza katika jibu la msingi kwamba kuna baadhi ya makusanyo na baadhi ya mapato mengine ambayo hayo tunahisi yanawezekana yakawa ni changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mchakato wa kuifanya NEMC kuwa NEMA kwa maana ya kuipa mamlaka na nguvu, huo mchakato umeshaanza na niwaombe tu Waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba mchakato huu unaendelea kwa sababu unapita kwenye hatua mbalimbali uakapokuwa tayari tutauleta hapa kwa ajili ya kuujadili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo mipango mbalimbali ambayo tumeipanga. Ni kweli zinatokea changamoto ndogondogo za upatikanaji wa vyeti, lakini nikwambie katika hili Mheshimiwa, Mameneja wetu wa Kanda, NEMC na Mkurugenzi wote wanafanya kazi kubwa na nzuri katika hili jambo kubwa la upatikanaji wa hizi certificate za tathmini na za ukaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninataka nichukue fursa hii niwapongeze sana wafanyakazi wote wa NEMC: Mkurugenzi na Mameneja wa Kanda kwa kazi kubwa wa wanayoifanya ya kuharakisha upatikanaji wa certificate hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto zinajitokeza, kwanza ni changamoto ya mifumo. Inafika wakati mifumo inakuwa inasumbua kwa hiyo kidogo inavuta muda. Changamoto nyingine ni kutokuwa na vigezo kwa baadhi ya miradi. Hatuwezi kutoa certificate kwa mradi ambao haujakidhi na haujatimiza vigezo. Hii ni kwa sababu ya kulinda mazingira na afya za wananchi, lakini zaidi taarifa za wataalam elekezi zinachelewa kuja kwetu. Tunawasajili wenyewe, lakini wawekezaji wakiwapa kazi ya kuandaa taarifa kuleta kwetu zinakuwa zinachelewa, mwisho wa siku mteja ama mwekezaji anakuwa anachelewesha katika upatikanaji wa certificate. Kwa hiyo, niwaombe tu wawekezaji wote wanapokuja kwetu wahakikishe kwamba tayari wameshakamilisha baadhi ya taratibu na vigezo ili tufanye haraka ya hivyo. Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, kuna mpango gani kutatua changamoto za NEMC hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini?

Supplementary Question 2

MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Je, kutokana na uchache wa mameneja wa kanda kama ulivyosema Mheshimiwa Waziri, sasa Serikali haioni haja kuwapa uwezo Mameneja wa Mikoa ili nao waweze kufanya shughuli ileile ambayo inafanywa na Mameneja wa Kanda ili kufanya zoezi lipate unafuu na liwe la haraka zaidi? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza. Nitumie fursa hii kwanza, nimpongeze sana kwa kazi kubwa anayoifanya hasa katika suala la hili la mazingira, amekuwa akishiriki kwenye program mbalimbali za uhifadhi hasa kule Zanzibar na maeneo mengine ya mikoa ya Tanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hapo katikati tulikuwa tuna changamoto ya uhaba wa Meneja wa kanda wa NEMC, lakini hapa karibuni tulifanya mabadiliko kidogo. Kwa mfano, Kanda ya Ziwa tulikuwa tuna mtu mmoja, Mheshimiwa Kayombo ndiyo meneja alikuwa kule. Tumeanza kugawa baadhi ya mikoa kwa maana kwamba, Mkoa kama wa Mara na mikoa mingine ya Katavi, tumeipunguza tumewapatia baadhi ya Meneja wengine wapya kwa ajili ya kusukuma hii kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie fursa hii niwapongeze sana Mameneja kwa kazi kubwa wanayoifanya ingawaje na uchache ambao wako nao. Tunao maafisa wetu viungo ukiacha Meneje wa Kanda ambao na wao wanaongeza kasi ya suala zima la uhifadhi na utunzaji wa mazingira hasa kwenye miradi mikubwa ikiwemo viwanda, migodi, majengo makubwa na miradi mingine ya uhifadhi wa vyanzo vya maji. Ninakushukuru.

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, kuna mpango gani kutatua changamoto za NEMC hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini?

Supplementary Question 3

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nipongeze Serikali kwa michakato inayoendelea ya kuibadili NEMC kuwa mamlaka. Je, ni lini Muswada wa Sheria wa kubadili Baraza la Mazingira kuwa mamlaka utauleta humu Bungeni?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Waheshimiwa Wabunge na Mheshimiwa Mbunge anafahamu kwamba, mchakato wowote wa mabadiliko ya sheria unapita hatua kwa hatua. Na tunafahamu mchakato huwa unakuja kwa sababu moja ni hiyo mahitaji kwamba, tunataka sasa tutoke katika hali hii tuende katika hali nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kama Ofisi ya Makamu wa Rais, hatua ya kwanza tayari tumeianza. Sasa tunasubiri hatua nyingine kutoka kwa mamlaka zenye uwezo zaidi pale zitakapofika. Wakati huo tumeshakuwa tayari kwamba sheria itakuja hapa na itajadiliwa. Wananchi wataona kazi kubwa inayofanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Taasisi ya Baraza la NEMC, na itakwenda kuwa mamlaka.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, kuna mpango gani kutatua changamoto za NEMC hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini?

Supplementary Question 4

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kutokana na tishio la climate change nchi nyingi duniani kwa mfano Brazil, Marekani na maeneo mengine wana Wizara ya Mazingira maalum. Suala hili limekuwa zito sana kwenye nchi yetu. Ni lini Wizara ya Mazingira itaanzishwa ili wataalam walioko kwenye maeneo mbalimbali wapewe nafasi ya kutumikia Wizara hii?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo la uanzishwaji wa Wizara ni jambo la kimamlaka zaidi. Kwa hiyo, nimuombe tu awe na subira mamlaka bila shaka itakuwa imemsikia itaona namna ya kufanya kwenye hili. Nakushuru ahsante.