Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 280 2025-05-12

Name

Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa kutatua tatizo la kukatika kwa umeme katika Jimbo la Kibiti?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inatekeleza mikakati mbalimbali ya matengenezo na ukarabati wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibiti ili kuondokana na tatizo la kukatika kwa umeme kunakotokana na uchakavu wa miundombinu hiyo. Mikakati hiyo ni kubadili nyanya za umeme kwa kuweka zenye uwezo mkubwa, kubadili nguzo za umeme na kuweka za zege, kubadili Pin insulators na kuweka mpya, na kufunga vidhibiti matatizo (kwenye line zenye urefu wa zaidi ya kilometa 50. Ahsante.