Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kutatua tatizo la kukatika kwa umeme katika Jimbo la Kibiti?

Supplementary Question 1

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina mambo mawili; kwanza, pongezi kwa Serikali kwa kazi kubwa na nzuri ambayo Daktari Samia Suluhu Hassan ameweza kuifanya na kutendea haki wananchi wa Jimbo la Kibiti hususan wale wanaoishi katika maeneo ya Delta Kata ya Kiungoroni, Mapaloni, Mbuchi, Msala kule kote kumepelekwa umeme takribani shilingi bilioni 3.8 tunashukuru sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja la nyongeza, kwa kuwa Serikali ilishatenga eneo pale kwenye Kata ya Ruwaruke Kijiji cha Lungungu kujenga substation ili kupunguza tatizo la kukatikakatika umeme. Sasa ni lini Serikali wataanza kufanya ujenzi huo?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge na nimpongeze amekuwa akifatilia jambo hili mara kwa mara. Pia tunashukuru kwa pongezi ambazo amezitoa kwa Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lake la kujenga Kituo cha Kupoza Umeme katika eneo la Lungungu ni kweli na sisi tulishafika katika eneo hilo na tulishafanya design na michoro ipo tayari. Ni kwamba tu Kituo cha Kupoza Umeme cha Lungungu lazima kilishwe na Kituo cha Kupoza Umeme cha Msifuni. Kwa hiyo, kwa sasa hivi ujenzi wa Kituo cha Umeme pale Msifuni kinaendelea Mkandarasi ni mzuri sana TIBEA na tuna uhakika atamaliza kazi kwa wakati. Akishamaliza pale tutajenga laini ya kutoka 400 kv mpaka 33 kv, msongo wa kilovoti 33 mpaka Lungungu kwa ajili ya kuweza kujenga kituo kidogo cha kupoza pale umeme ili wananchi wa Kibiti na wenyewe waendelee kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Mbunge avute subira, mikakati imeanza kupitia kituo cha kupoza umeme kikubwa cha Misifuni ambacho kitaenda kulisha Lungungu pale ambapo mradi utakamilika basi tutajenga na hicho Kituo kidogo cha Kupoza Umeme Lungungu. Ahsante.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kutatua tatizo la kukatika kwa umeme katika Jimbo la Kibiti?

Supplementary Question 2

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, transfoma iliyopelekwa na Mkandarasi katika Kijiji cha Kigulunde Kata ya Ngwelo iliungua na ninavyosema sasa hivi ni miezi minne hawapati huduma. Je, nini kauli ya Serikali ya kumtaka Mkandarasi yule kupeleka transfoma nyingine ili wananchi wangu waondokane na adha wanayoendelea kuipata sasa? Ninakushukuru.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpe pole Mheshimiwa Shekilindi na wananchi wa Kijiji hiki cha Kigulunde kwa changamoto ambayo wameipokea. Ninaomba nikitoka hapa nifuatilie ili tuhakikishe kwamba tatizo hilo linatatuliwa na wananchi wake wa Kijiji cha Kigulunde waendelee kunufaika na upatikanaji wa umeme katika kijiji hicho. Kwa hiyo, nikitoka hapa Mheshimiwa Mbunge nitafuatilia tuweze kutatua changamoto hiyo.

Name

Philipo Augustino Mulugo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songwe

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kutatua tatizo la kukatika kwa umeme katika Jimbo la Kibiti?

Supplementary Question 3

MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Songwe kwa ujumla wake, umeme kwa sasa unakatikakatika mara kwa mara na wachimbaji wadogo wa Saza, Makangorosi, Chunya, Mbangala, Patamela wanapata hasara sana kwa ajili ya mota zao zinaharibika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tunashukuru sana Serikali kwa kuleta umeme vijiji vyote vya Wilaya ya Songwe, lakini kwa kweli tatizo kubwa ni kukatikakatika kwa umeme hasa kwenye viwanda vidogo vya makarasha. Nini kauli ya Serikali?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ninaomba nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake na kwa kweli amekuwa akifuatilia mara kwa mara kuweza kuona namna ya kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Songwe. Serikali kupitia Wizara ya Nishati tunatekeleza mradi mkubwa wa kupeleka umeme katika Mikoa ya Songwe hadi kufika katika Mkoa wa Rukwa kwa maana ya kupeleka gridi katika Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mradi huu tunajenga vituo vya kupoza umeme maeneo mbalimbali ikiwemo, katika Mkoa wa Songwe. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge, mradi huu unaendelea na mkandarasi kwa kweli ana-speed nzuri sana. Tuombe watuvumilie, tutakapokamilisha kujenga Kituo cha Kupoza Umeme pale Songwe, basi tutakuwa tumeimarisha hali ya upatikanaji wa umeme pale na wananchi hususan hawa ambao wapo katika machimbo, wachimbaji wadogo wa madini na wenyewe wataweza kunufaika kwa sababu umeme utaendelea kuwa wa uhakika zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mradi unaendelea na uko hatua nzuri, tuwaombe wananchi wa Songwe kupitia Mheshimiwa Mulugo waendelee kutuvumilia wakati Mkandarasi yuko site na atamaliza. Tulikubaliana mpaka Mei, 2026 lakini kwa kasi ya Mkandarasi huyu tuna uhakika ataweza kusogeza muda nyuma kidogo ili wananchi hawa waendelee kunufaika. Ahsante.