Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 22 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 281 | 2025-05-12 |
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-
Je, lini ukarabati na upanuzi wa Mradi wa Maji Makonde utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Makonde kupitia Mradi wa Maji wa Miji 28 kwa gharama ya shilingi bilioni 84.7. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu vitatu vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 26 kwa siku, ujenzi wa matanki manne yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 13 na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 81.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 37% ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2025 na kunufaisha wananchi waishio kwenye Wilaya za Newala, Tandahimba pamoja na Mji wa Nyanyamba.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved