Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 22 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 282 | 2025-05-12 |
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE K.n.y. MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha Miradi ya Maji ya Rukoma na Mwakizega – Uvinza?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji Mwakizega uliopo Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma. Kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 300,000, ulazaji wa bomba umbali wa kilometa 21.5 sanjari na ujenzi wa vituo 46 vya kuchotea maji. Mradi huo umefikia wastani wa 85% na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na kunufaisha zaidi ya wananchi 20,348 waishio katika vijiji vya Mwakizega pamoja na Kabeba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) itakarabati miundombinu chakavu ya Mradi wa Maji wa Rukoma pamoja na kuongeza wingi wa maji kwa kufanya upanuzi wa kutoa maji Kijiji cha Lagosa kwenda Rukoma kupitia Skimu ya Maji ya Buhingu. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved