Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE K.n.y. MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha Miradi ya Maji ya Rukoma na Mwakizega – Uvinza?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Jimbo la Kigoma Kusini kwa eneo kubwa limepakana na Ziwa Tanganyika, lakini pia na Mto Malagarasi. Vipo vijiji ambavyo vimepakana kabisa na Ziwa Tanganyika, wananchi wanakwenda kuchota maji kwa kutumia ndoo kwenye Ziwa Tanganyika, lakini havina maji. Ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha vijiji hivyo vinavyopakana na Ziwa Tanganyika vinapatiwa maji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; katika Halmashauri ya Kasulu DC Kata ya Muzye lilijengwa tenki linalohifadhi maji kiasi cha lita 250 lakini mpaka sasa hakuna mabomba yanayopelekwa pale kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji. Je, ni lini Serikali itapeleka Mkandarasi ipeleke na mabomba ili kumaliza tatizo kusudi wananchi waondokane na tatizo la maji? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru sana Wanakigoma. Mheshimiwa Rais katika bajeti ya 2024/2025 ambayo inahitimishwa mwezi ujao, takribani shilingi bilioni 13.9 zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya Mkoa wa Kigoma na zaidi ya miradi 37 imetekelezwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kipindi cha 2024/2025. Hii ni dalili tosha kabisa kwamba Mheshimiwa Rais yupo committed sana kuhakikisha kwamba Wanakigoma wanapata suluhisho la maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye Ziwa Tanganyika, chanzo cha uhakika cha maji katika Mkoa wa Kigoma, Rukwa pamoja na Katavi ni Ziwa Tanganyika. Pia, hata uchakataji wa maji mpaka yamfikie mtumiaji ambao ni wenye gharama nafuu zaidi ni Ziwa Tanganyika na ndiyo maana Mheshimiwa Rais amesharidhia na akatoa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaanza kufanya study, wataalam wetu wanapita huko kuanzia Katavi, Rukwa pamoja na Kigoma ili tuone namna gani tutajenga mradi mkubwa wa kimkakati wa kuhakikisha kwamba wananchi wanaoishi katika maeneo ya pembezoni mwa Ziwa Tanganyika waanze kuwa wanufaika wa kwanza wa kupata huduma ya maji safi na salama kabla hatujayapeleka maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimtoe hofu, Serikali ipo kazini inafanya kazi nzuri kabisa na kwa bajeti hii ya shilingi trilioni 1.016 mliyoipitisha siku ya Ijumaa hakuna ambalo litashindikana. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, vijiji hivi vitakuwa sehemu ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa eneo la pili, tumeshajenga tenki na sasa yamebaki mabomba. Nimhakikishie kwamba hatuwezi kujenga tenki halafu tukaacha kupeleka mabomba kwa sababu maji lazima yapitie kwenye mabomba ili yawafikie watumiaji. Ninalichukua kwa uzito stahiki, nitaenda kulifanyia kazi na nitampa mrejesho wa nini tunaenda kukifanya. Lengo wananchi wetu na wananchi ambao Mbunge anawapambania wapate huduma ya maji safi na salama. Ninashukuru sana. (Makofi)

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE K.n.y. MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha Miradi ya Maji ya Rukoma na Mwakizega – Uvinza?

Supplementary Question 2

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Tunaishukuru sana Serikali kwa kuchimba visima 12 katika Jimbo la Mbulu Mjini na hadi sasa visima sita bado havijakamilika na hata tukitangaza mara kadhaa Wakandarasi huwa hawaombi. Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuhakikisha walau wakandarasi wanalipwa ili waweze kuomba kazi pale inapotangazwa? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa changamoto hizi tunakutana nazo na kuna maeneo ambayo mfano hata Singida tumekutana na wakandarasi akapatikana wa kwanza akafanya akashindwa, akaja wa pili akashindwa. Ni uwezo tofauti wa kifedha wa kuhimili kuwa na vifaa na mashine za nguvu ambazo zinaweza kuhimili maeneo mbalimbali. Kwa hiyo tunatambua kabisa kwamba maeneo hayo mara nyingine tunachimba hata maji hatupati lakini kuna maeneo ambayo unapata, lakini inahitaji vifaa ambavyo vina gharama kubwa zaidi, lakini unaenda kutekeleza mradi wenye gharama ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hapa ndiyo kumekuwa na changamoto kubwa. Sasa Serikali ndiyo maana ikaona kwamba tutanunua mitambo yetu. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atanunua mitambo 25 ya kuchimbia visima hivyo, lakini bado tunapitia changamoto mbalimbali. Serikali imeshaanza kuangalia kutumia vyanzo vingine ili kusogeza maji katika maeneo ambayo sasa tumeshindwa kuchimba kisima. Lengo kubwa ni kwamba wananchi wanahitaji huduma ya maji safi na salama. Nimtoe hofu maeneo hayo tutayafikishia maji na kwa Serikali hii maji yatafika katika eneo hilo na wananchi wa Mbunge watapata huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.