Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 283 2025-05-12

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:-

Je, Serikali imetoa fedha kiasi gani za ujenzi wa Bandari Kavu katika Mji wa Tunduma ambayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) imeainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 1,600 katika Kijiji cha Mpemba Mkoani Songwe litakalotumika kujenga Bandari Kavu ambayo itahudumia maeneo ya mipakani ikiwemo Tunduma. Kwa sasa hatua iliyofikiwa ni taratibu za utwaaji wa ardhi ili kuruhusu mipango ya ujenzi wa bandari hiyo hivyo, gharama halisi zitajulikana baadaye, ahsante. (Makofi)