Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, Serikali imetoa fedha kiasi gani za ujenzi wa Bandari Kavu katika Mji wa Tunduma ambayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaishukuru Serikali kwa kulipa fidia kwa wananchi, lakini ninataka kufahamu, ni lini hasa Serikali imepanga kuanza ujenzi wa hii Bandari Kavu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu namba mbili; sambamba na ujenzi wa Bandari Kavu, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha unaboresha Reli ya TAZARA?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Neema Mwandabila, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, tunakamilisha taratibu zote za kutwaa lile eneo. Taratibu zikishakamilika sasa kujua tarehe ni lini itategemea na mchakato utakavyokuwa umekamilika lakini azma ya Serikali ni kuanza ujenzi haraka kadri Serikali itakavyokuwa imekamilisha utwaaji wa hilo eneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo tunajua kwamba Bandari Kavu hiyo inajengwa kwa sababu ya kuunganisha hiyo Bandari Kavu na Bandari ya Dar es Salaam kupitia Reli ya TAZARA. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba hata katika ziara aliyofanya Mheshimiwa Rais kwenda China, tayari kuna makubaliano maalum ya kuhakikisha kwamba Reli ya TAZARA inafanyiwa ukarabati mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika hata katika bajeti itakayokuja ya Uchukuzi, Waheshimiwa Wabunge watapata bahati ya kuisikia, lakini mpango wa Serikali ni kuifanyia ukarabati mkubwa ili irudi kwenye hali yake ya ubora na ndiyo, maana Serikali imeamua kuwekeza vikubwa katika hiyo Bandari Kavu ya Mpemba ambayo iko mpakani kabisa mwa nchi yetu na nchi ambazo tunafanya nazo biashara ikiwepo ya Malawi, Zambia, DRC mpaka Zimbabwe.

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, Serikali imetoa fedha kiasi gani za ujenzi wa Bandari Kavu katika Mji wa Tunduma ambayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 2

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kauli ya Serikali juu ya Ujenzi wa Bandari Kavu katika Mkoa wa Tabora? Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bandari Kavu ni kusogeza huduma za bandari kwenda sehemu za nchi kavu. Kwa sasa tuna bandari ambayo inafanya kazi eneo la katikati ambalo ni Isaka, lakini kwa upande wa Mkoa wa Tabora tathmini lazima ifanyike. Kwa sababu MGR ipo (hiyo Reli ya Kati ya Zamani) lakini pia hii Reli ya SGR. Kwa hiyo lazima tathmini ifanyike kuonekana kwamba kuna umuhimu wa kujenga Bandari Kavu katika Mkoa wa Tabora. (Makofi)