Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 284 2025-05-12

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-

Je, kuna sera za Vipaumbele kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika miradi ya serikali?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI: alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Uchukuzi ya Mwaka 2003 imetoa kipaumbele cha kutambua na kutatua changamoto mbalimbali za wanawake katika kuleta usawa katika jamii. Kwa kupitia Miradi ya Usafirishaji inayotekelezwa na Serikali, wanawake wajasiriamali wamepewa nafasi za kuwezeshwa kufanya biashara katika Vituo vya Reli ya SGR Dar es Salaam – Dodoma. Pia, vituo vya mabasi ya Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha na Mikoa mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanawake wajasiriamali ambao ni madereva wa vyombo vya usafiri wanatoa huduma za usafiri katika vituo hivyo na maeneo ambayo miradi ya Serikali inaendelea kutekelezwa ambapo wamethibitishwa na kusajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Ahsante.