Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:- Je, kuna sera za Vipaumbele kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika miradi ya serikali?

Supplementary Question 1

MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nilikuwa na maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ni hatua gani mahususi ambazo Serikali imezifanya kuhakikisha wanawake wajasiriamali wanahusika moja kwa moja katika miradi ya uchukuzi hususan kwenye ununuzi wa magari na zabuni za usafiri wa umma? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; mikakati gani maalum ambayo Serikali imejiwekea kuhakikisha wanawake wajasiriamali wanaweza kupata fursa za kiuchumi katika miradi ya usafirishaji hasa kwa kuwapa semina? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge yote mawili kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibu la msingi; kwanza Sera ipo ya kuhakikisha kwamba wanawake wanapewa kipaumbele katika shughuli za miradi mbalimbali ya kufanya shughuli zao katika Sekta ya Uchukuzi. Ndiyo maana kama nilivyosema sasa hivi katika miradi ambayo tumeweka ipo miradi ambayo imetengwa kwamba hii lazima itashughulikiwa na wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hiyo miradi iliyotengwa bado pia wanashindanishwa katika miradi yote ya kawaida. Kwa hiyo kwa sababu Sera ipo na miradi hiyo tumeshatenga pia nafasi zao, kwa hiyo, hiyo ndiyo mikakati ya Serikali. Sera ipo, lakini pia Wabunge wakienda sasa hivi kwenye miradi ambayo tunatekeleza na hasa ya SGR wapo wanawake wengi ambao wanaendesha shughuli zao kwa sababu ya hiyo Sera, lakini ni pamoja na nafasi ambayo Serikali imetoa.