Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 287 2025-05-12

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:-

Je, lini Serikali itakomesha wizi wa mtandao kupitia Sim Banking na ni wahalifu wangapi wamekamatwa na hatua gani zimechukuliwa?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeendelea kukua kwa kasi hapa nchini na duniani kwa ujumla na kusababisha kuimarika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na hata kisiasa. Miongoni mwa maeneo yaliyofaidika ni pamoja na huduma za fedha. Kwa mujibu wa takwimu za TCRA za robo ya tatu ya huu mwaka wa fedha 2024/2025, idadi ya laini za simu imefikia milioni 90.4 na utumiaji wa internet umefikia milioni 49.3. Mafanikio haya yamekuja na fursa na changamoto mbalimbali, ikiwemo wizi wa mitandaoni ukihusisha pia, Sim Banking ambapo watumiaji wa huduma za mawasiliano wamekuwa wakifanyiwa hadaa na kujikuta wametapeliwa fedha zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na changamoto hizi Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Mawasiliano Nchini imeendelea kuelimisha umma kuhusiana na masuala mbalimbali ya usalama mtandaoni kwa kupitia kampeni mbalimbali, ikiwemo Kampeni ya SITAPELIKI pamoja na NIRAHISI SANA, ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu namna bora na salama ya kutumia mitandao, ikiwemo utunzaji wa nywila, kuwa na nywila imara katika programu mbalimbali za kifedha na zile za matumizi mengine. Aidha, kwa upande mwingine Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeendelea kujiimarisha katika aina hizi mbaya za uhalifu na tayari hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kwa wahalifu. Ahsante. (Makofi)