Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Je, lini Serikali itakomesha wizi wa mtandao kupitia Sim Banking na ni wahalifu wangapi wamekamatwa na hatua gani zimechukuliwa?
Supplementary Question 1
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa maelezo yake mazuri, ambayo yametoa faida kwa jamii. Nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, mitandao inasaidia kupata mawasiliano ya haraka, lakini utakuta pia, inakera katika taarifa hizo za haraka kwa sababu, unaweza ukaletewa jambo kila ukikaa linarudia hilohilo. Je, kama hilo jambo mie sitaki lirejee tena kwenye simu yangu nifanye nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti swali la pili. Unasema kwamba, wahalifu wanachukuliwa hatua. Hatua gani kwa sababu, taarifa zake wananchi hawazipati. Uzuri wa taarifa na hatua kwamba, mzitangaze, ili tujue mtu fulani kafanya kitu fulani, kachukuliwa hatua fulani. Je, hizi taarifa tutazipata vipi? Ahsante. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipokee pongezi zako Mheshimiwa Fakharia, lakini kwenye suala la messages zinajirudia rudia; messages zinapojirudiarudia, elimu tunayoendelea kuitoa kwa wananchi ni tunaomba sana, kwa kutumia Bunge lako Tukufu, wananchi wote lazima wawe kwanza na mawasiliano na watu wanaowafahamu na kama unapata message ya mtu, ambaye humfahamu ni vyema ukapuuza. Usipende kufanyia kazi message ambayo mtu humfahamu. Watu wengi wanaotapeliwa ni wale wanaojihusisha na kusikiliza mtu ambaye hamfahamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, unaambiwa unatakiwa kupata milioni sita, tuma namba hii, jibu swali hili. Usipende fedha za kirahisi kwa sababu, pamoja na changamoto za ugumu wa maisha hakuna fedha ya rahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kupata vitu vya kirahisi, kwa mfano, Waheshimiwa Wabunge hapa, wengi tumetapeliwa kwa kudhania kwamba, tuna majiko ya gesi ambayo utapatiwa, kuna watu fulani wanataka wakupatie majiko ya gesi. Sasa wewe kwa nini ujihusishe na mtu ambaye humfahamu! Unamtuamia mtu 400,000 ili usafirishiwe majiko ambayo hayapo kwenye utaratibu rasmi. Kwa hiyo, wito wangu kwa wananchi wote ni kuona kwamba, kila mmoja ahakikishe anawasiliana na mtu anayemfahamu na kama humfahamu ninakushauri upuuze. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua zinazochukuliwa na sisi, kama Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kupitia Taasisi yetu ya TCRA. Kazi kubwa tunayoifanya ni kutambua, kupitia mitambo tuliyonayo. Tukishatambua, tunawakabidhi wenzetu wa Jeshi la Polisi, wao sasa wanafanya taratibu zao za Kisheria, kadiri ambavyo nchi yetu inaendeshwa Kisheria. Wengi wameshafikishwa Mahakamani na wameshafungiwa hizo line, nyingi sana zimeshafungiwa, na hawa wanaochipukia, sisi kama Serikali tutaendelea kuwafanyia kazi. Ahsante. (Makofi)
Name
Maulid Saleh Ali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Welezo
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Je, lini Serikali itakomesha wizi wa mtandao kupitia Sim Banking na ni wahalifu wangapi wamekamatwa na hatua gani zimechukuliwa?
Supplementary Question 2
MHE. MAULID SALEH ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, malalamiko mengi ya wizi mitandaoni yanaelekezwa kwenye Jeshi la Polisi. Je, Serikali haioni haja ya kuwapatia access (database) ya moja kwa moja, ili tukio lolote la kihalifu linapotokea waweze kuchukua hatua za haraka zaidi? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza, Jeshi la Polisi kupata access; ninachoweza kusema ni sisi, kama Serikali, Jeshi la Polisi siyo kwamba, halina access, lakini Serikali inafanya kazi kama timu moja. Kwa hiyo, wao wanafanya kwenye sehemu yao na sisi kama TCRA kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na yenyewe pia, inafanya sehemu yao. Tutaendelea kuboresha Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba, mifumo inakuwa mizuri zaidi ya ambavyo ipo sasa. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved