Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 288 2025-05-12

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali yenye urefu wa kilometa 35 utakamilika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza maandalizi, kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Katoma – Bukwali, yenye urefu wa kilometa 35, kwa kuanza kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kazi hiyo ilianza Machi 2024 na inatarajiwa kukamilika Septemba 2025. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha, kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.