Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali yenye urefu wa kilometa 35 utakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nichukue fursa hii kuipongeza Serikali ya Dkt. Samia kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikipaza sauti juu ya barabara hii na sasa tunaona imefikia hatua kubwa ya kuiweka kwenye upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ili tuweze kupata bajeti, kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo. Katika majibu ya swali la msingi ni kwamba, barabara hiyo upembuzi utaisha Septemba, 2025. swali la kwanza; je, sasa Serikali haioni haja ya kuweka kwenye bajeti, angalau baada ya Septemba tuweze kupata kiasi cha fedha ianze kujengwa kwa kiwango cha lami tukisubiri mwaka wa fedha mwingine unaofuata? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; Barabara nyingine ya Omushenyi – Bugandika – Kitobo – Buyango – Ruzinga na yenyewe ni barabara ambayo inahudumiwa na TANROADS. Je, ni lini barabara hiyo na yenyewe itawekwa katika utaratibu wa usanifu na upembuzi yakinifu ili na yenyewe ianze kujengwa katika kiwango cha lami? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa, ambayo anaifanya hadi barabara hii imeingia kwenye utaratibu wa kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kama tulivyosema kwenye jibu la msingi, usanifu utakamilika mwaka huu 2025, mwezi Septemba na kwa taratibu zetu ni kwamba, bajeti tumeshaipitisha, kwa ajili ya usanifu. Pia, tunaamini kwamba, kwa kuwa, tutakuwa tumekamilisha, basi katika mwaka unaofuata itaingizwa kwenye mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami kwa sababu, tutakuwa tayari tumeshakamilisha usanifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hii Barabara ya pili, ambayo anasema inaanza Omushenye kwenda Ruzinga, ni barabara ambayo pia, tunaihudumia, lakini ni Barabara ya Mkoa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutakachokifanya kwa sasa ni kwamba, tutahakikisha inapitika kipindi chote cha mwaka, lakini tayari tukiwa tunafikiria kuiweka kwenye maandalizi ya kuifanyia pia, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa mwaka wa fedha utakaofuata. Ahsante. (Makofi)

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali yenye urefu wa kilometa 35 utakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Jimbo la Mtwara Vijijini linapakana na Nchi ya Msumbiji na tuna barabara zetu za ulinzi. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha barabara hizi muhimu za ulinzi zinajengwa kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna barabara ndefu sana, ambayo inaambaa ambaa na Mto Ruvuma, tayari tumeshaanza, ili ipitike muda wote. Barabara ambayo ipo chini, lakini tumeanza kujenga madaraja makubwa karibu yote kuhakikisha kwamba, inapitika kwa sababu, kipindi cha masika huwa inashindwa kupitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya pili, na hata katika Sera yetu ya Ujenzi, ni kwamba moja ya kipaumbele ni kujenga hizi barabara za za mipakani, kuziimarisha, ikiwa ni pamoja na kuzijenga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, wakati tunaimarisha kuijenga na kujenga madaraja, tayari tuna mpango wa kutaka kuanza kuijenga yote kwa kiwango cha lami, lakini kwanza tuhakikishe kwamba inapitika muda wote wa mwaka, ahsante. (Makofi)

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali yenye urefu wa kilometa 35 utakamilika?

Supplementary Question 3

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa ujenzi wa Daraja la Rau ulifungua ile barabara na Mheshimiwa Naibu Waziri alikuwepo alipokuja Mheshimiwa Rais, je, ni lini sasa ile Barabara ya Rau – Shimbwe, Rau – Kishumundu ambako ndiyo wengi mnaifahamu sana Kishumundu, pia na barabara ile ya Old Moshi Magharibi na Old Moshi Mashariki zitapata ujenzi wa lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nijibu maswali yake kuhusu barabara hizo mbili. Ni kweli, kwanza ni maombi ya mkoa, lakini pia ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali inatafuta fedha kuhakikisha kwamba barabara hiyo tunaijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoma – Bukwali yenye urefu wa kilometa 35 utakamilika?

Supplementary Question 4

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Jimbo la Mtwara Mjini linapakana na eneo moja linaloitwa Mnazi Bay kwenye visima vya gesi, je, ni lini Serikali itatuwekea lami kutoka Mtwara Mjini mpaka kwenye visima hivi vya gesi? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, lakini kwa maana ya ubaya na isiyopitika, kwanza ninatoa maelekezo kabisa kwa Meneja wa Mkoa wa Mtwara kuhakikisha kwamba barabara hii ambayo inakwenda kwenye maeneo ya kimkakati inatengenezwa na kupitika kipindi chote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara hii ipo kwenye mipango yetu kuijenga kwa kiwango cha lami kwa sababu tayari ilishafanyiwa usanifu, ahsante.