Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 23 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 289 | 2025-05-13 |
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:-
Je, Serikali imefikia wapi kufuatilia kesi inayomkabili Human Resources Manager wa Kampuni ya Dangote Cement Mtwara?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilifanya ukaguzi maalum katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa Sheria za Kazi, ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Ajira za Wageni, Sura 436. Aidha, ukaguzi huo haukuweza kupata ushahidi kuhusu uwepo wa kesi inayomkabili Meneja Rasilimali Watu, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved