Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:- Je, Serikali imefikia wapi kufuatilia kesi inayomkabili Human Resources Manager wa Kampuni ya Dangote Cement Mtwara?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa, imekuwa ni kawaida kwa wageni wengi katika eneo hili la utawala (Human Resource Management), kutokana na asili ya nchi zao, wanapotoka huwa hawafahamu vizuri taratibu ambazo ILO inazisimamia. Je, Serikali haioni kwamba ni busara sasa nafasi hii muhimu sana katika nchi yetu isiwe inatolewa kwa wageni? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Shangazi ametoa ushauri kwa Serikali, lakini kimsingi kwa mujibu wa sheria, ipo hivyo kwa maana ya wageni hawaruhusiwi kushika hizi nafasi za Afisa Rasilimali Watu, kwa maana wiki iliyopita Mheshimiwa Waziri wa Kazi alikutana na Menejimenti ya Dangote pale ofisini, na wakajadiliana jambo hili kwa kina, na baadaye wakajiridhisha pasipokuwa na shaka kwamba, huyu mhusika ambaye ametajwa hapa kwamba ni Afisa Rasilimali Watu, hakuhusika moja kwa moja kwenye eneo hilo, na badala yake yupo Mtanzania ambaye anahudumu katika nafasi hiyo. Nakushukuru sana.