Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 290 2025-05-13

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE K.n.y. MHE. ALFRED J. KIMEA aliuliza:-

Je, lini Serikali itazipandisha hadhi Sekondari za Ngombezi, Joel Bendera na Kwamndolwa, Korogwe TC, kuwa za kidato cha tano na sita?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule za Sekondari Ngombezi, Joel Bendera na Kwamndolwa ni shule zilizo kwenye mpango wa kupandishwa hadhi na kuwa za Kidato cha Tano na Sita. Shule hizi zimejengewa baadhi ya miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita. Hivyo, shule hizi zitapandishwa hadhi pindi zitakapokidhi vigezo. Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ili kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule za Sekondari Ngombezi, Joel Bendera na Kwamndolwa kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha.