Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE K.n.y. MHE. ALFRED J. KIMEA aliuliza:- Je, lini Serikali itazipandisha hadhi Sekondari za Ngombezi, Joel Bendera na Kwamndolwa, Korogwe TC, kuwa za kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 1
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa, tumejenga shule za sekondari nyingi katika maeneo yetu na watoto wamekuwa wengi sana, hasa wa form four, ni lini Serikali itaweka mikakati kuhakikisha tunaongeza A’ Level katika maeneo yetu hayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa kuwa, Jimbo la Nsimbo napo kuna shule za sekondari nyingi na high school zipo shule mbili tu, na shule za sekondari zipo kama 22, ni lini Serikali itatuongezea high schools katika Halmahsauri yetu ya Nsimbo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa sana katika kuhakikisha kwamba elimu msingi inaendelea kuimarika. Imekuwa ikifanya hivyo kwa kuboresha miundombinu na sekta nzima, kwa maana ya kupata walimu, vifaa na mazingira yote ambayo yanawezesha elimu yetu ya msingi kuimarika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la Mheshimiwa Mbunge, naomba nijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja kwamba Serikali katika kipindi cha miaka minne tayari imeshajenga mabweni 738. Kama sote tunavyofahamu, shule nyingi za kidato cha tano na sita ni Shule za Kitaifa na hivyo zinakuwa ni shule za bweni. Kwa hiyo, kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu muhimu, ikiwemo mabweni, tayari tumeweza kupandisha hadhi shule hizi za kidato cha nne kuwa sasa zina hadhi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kufanya jitihada hizo kwa kuendelea, siyo tu kujenga Shule za Sekondari za Kata, lakini kuendelea kupandisha hadhi baadhi ya shule hizi za kata, kuzijengea miundombinu ambayo itawezesha kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa muktadha huo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika Jimbo la Nsimbo tutaendelea na jitihada hizo za kuendelea kuongeza shule za kidato cha tano na sita.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE K.n.y. MHE. ALFRED J. KIMEA aliuliza:- Je, lini Serikali itazipandisha hadhi Sekondari za Ngombezi, Joel Bendera na Kwamndolwa, Korogwe TC, kuwa za kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 2
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Shule ya Sekondari Inchugu na Nyanungu zimepandishwa hadhi tangu mwaka 2024. Kuna mabweni mawili yamekamilika, madarasa zaidi ya sita yamekamilika, matundu ya vyoo yamekamilika, vitanda vimewekwa katika mabweni yote. Sasa ni lini wanafunzi watapelekwa Inchugu High School na Nyanungu ili watoto wasiende umbali mrefu, wakae pale pale shuleni wapate elimu nzuri? Ahsante
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Waitara kwamba kama nilivyotangulia kusema, Serikali pamoja na kwamba inaendelea kuhakikisha tunafikia kata mbalimbali nchini ambazo hazina shule za sekondari na kuzijengea shule hizi pia, tunafanya jitihada ya kupandisha hadhi baadhi ya hizi shule ili ziweze kuchukua wanafunzi wa Kidato cha tano na sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika shule ambazo Mheshimiwa Waitara amezitaja, hizi mbili ambazo amekiri kwamba miundombinu ni toshelezi sasa kuweza kupandishwa hadhi na kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni taratibu tu, lakini tutakamilisha taratibu hizo haraka iwezekanavyo ili sasa wanafunzi wetu wa kidato cha tano na sita waweze kuanza kusoma katika hizi shule mbili ambazo amezitaja. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved