Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 291 2025-05-13

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELO aliuliza:-

Je, sababu zipi zinasababisha Mikopo ya Wanawake kuchelewa kutolewa kwa waliokidhi vigezo vyote, hasa Wanawake wa Mkoa wa Mwanza?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Halmashauri za Mkoa wa Mwanza inaendelea kutekeleza jukumu la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake waliokidhi vigezo kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo za Mwaka 2024.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo hiyo hutolewa kwa utaratibu mahususi unaolenga kuhakikisha uwazi, usawa na ufanisi katika usimamizi wa fedha hizo. Kwa mujibu wa kanuni hizo, Serikali za Mitaa hushughulikia maombi ya mikopo yanayowasilishwa katika ngazi ya kata na kufuata hatua muhimu, ikiwemo uchambuzi wa vikundi, ukaguzi wa miradi, tathmini ya maombi, uhakiki wa taarifa na utoaji wa mafunzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato huu unatekelezwa ndani ya siku 60 tangu tarehe ya mwisho ya kupokea maombi, ambayo hupokelewa ndani ya siku 30 baada ya kutolewa kwa tangazo. Hali hii husababisha kuchelewa kwa utoaji wa mikopo, siyo kwa nia ya kuwanyima fursa wanawake, bali kwa madhumuni ya kuhakikisha utaratibu wa utoaji wa fedha hizi unafanywa kwa usahihi na kwa vikundi vilivyo tayari kutekeleza miradi kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa kutambua hilo, imeendelea kutoa elimu, kuimarisha mifumo na taratibu za utoaji mikopo ili kupunguza ucheleweshaji usio wa lazima.