Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 292 2025-05-13

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha kimkakati kwenye Kata ya Lukozi – Lushoto?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetenga shilingi bilioni 53.5 kupitia Bajeti ya Nyongeza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 214 katika Kata za Kimkakati kote nchini ikiwemo Kata ya Lukozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Kata ya Lukozi imetengewa shilingi milioni 250 na tayari Serikali imeanza kupeleka fedha hizo kwa awamu ya kwanza katika majimbo 120.