Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha kimkakati kwenye Kata ya Lukozi – Lushoto?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali. Kwanza nitumie fursa hii kuipongeza sana Serikali kwa kupeleka fedha kwenye Kituo cha Afya Lukozi, kituo ambacho kinahudumia wananchi wengi sana takribani Tarafa nzima ya Mlalo. Naishukuru sana Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja tu la nyongeza. Kituo cha Afya Pagwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi nimeshauliza hapa mara kadhaa namna ambavyo Serikali inakichukua kama kituo cha kimkakati na kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wake ili kuokoa akina mama ambao wanapata shida ya kufuata huduma za afya katika hospitali ya halmashauri ambayo ipo mbali sana na kata hii. Je, nacho kimepata fedha hizi au Serikali ina mkakati gani wa kuweza kukiwezesha na chenyewe kupata fedha na kuweza kujenga kituo hiki? Nashukuru sana. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Husna Sekiboko kwa swali lake hili linalolenga kuimarisha sekta ya afya msingi, na hususan akiwazungumzia akina mama ambao anataka wapate huduma bora zaidi za afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake hili moja, naomba kumpatia taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kabisa kuhakikisha kwamba inaendelea kuimarisha sekta ya afya msingi, ndiyo maana katika kipindi cha miaka minne utaona kwamba jumla ya vituo vya afya 367 vimejengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na mikakati hiyo ya kuboresha miundombinu muhimu katika sekta hii ya afya msingi kwa kujenga siyo tu vituo vya afya, bali pia ni pamoja na kuhakikisha kila halmashauri inakuwa na hospitali ya halmashauri na kuendelea kujenga zahanati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la kituo hiki mahsusi alichokitaja, naomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, kama tayari kituo hiki cha afya kwenye Kata ya Lukozi katika mwaka huu wa fedha kimepelekewa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu muhimu kabisa, nimhakikishie kwamba Serikali itaendelea kuleta fedha katika Mkoa wa Tanga katika jimbo hili la Lushoto, kuhakikisha kwamba inaendelea kujenga vituo vya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo tu vituo vya afya, bali pia vituo vya kutolea huduma ya afya msingi ikiwemo kituo cha afya alichokitaja Mheshimiwa Husna Sekiboko.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved