Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 293 2025-05-13

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vipaumbele muhimu vya Serikali katika kuboresha huduma za afya ni magari ya wagonjwa na magari ya usimamamizi wa huduma za afya. Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilinunua magari 594 na kuyapeleka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ilipelekewa magari matatu ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Hospitali ya Kinyonga, Kituo cha Afya Chumo na Njinjo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya afya vyenye uhitaji kote nchini, kikiwemo kituo cha afya Nanjirinji.