Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, na pia nashukuru na kuipongeza Serikali yangu kwa hatua hii ya kupeleka magari ya kubebea wagonjwa kwenye vituo vyetu vya afya. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kutokana na ukweli kwamba baadhi ya vituo vya afya kikiwemo Nanjirinji vipo mbali na ni vigumu kufikika kutoka kwenye hospitali zetu, hasa za wilaya, je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka magari ya wagonjwa kwenye vituo kama Nanjirinji kutokana na hali hii ya ugumu wa kufikika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa muktadha huo huo, je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kupeleka magari ya wagonjwa kwenye vituo vyote, ifanye assessment vituo vyote ambavyo ni vigumu kufikika nchini ili magari haya yapelekwe katika maeneo yote nchini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Ally Kassinge kwa swali lake zuri ambalo linalenga kuendelea kuzungumzia uimarishaji wa sekta ya afya msingi. Naomba nijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja kwamba, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa kuwa na magari ya kubebea wagonjwa pamoja na magari ya usimamizi wa huduma za afya. Ndiyo maana katika mwaka wa bajeti 2021/2022 Serikali ilinunua magari 594 ya kubebea wagonjwa pamoja na ya usimamizi wa huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magari haya yamesambazwa kote nchini katika vituo ambavyo vina mahitaji makubwa. Katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, kama nilivyotangulia kujibu kwenye majibu ya msingi, magari matatu yamepelekwa kwa ajili ya kutoa huduma hizo muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kumuakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwamba kama vile Serikali ilivyoanza na jitihada ya kununua haya magari 594, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kununua magari mengine na kuyasambaza kote nchini kwa ajili ya kwenda kutoa huduma muhimu kabisa hizi za kubeba wagonjwa pamoja na usimamizi wa huduma za afya. Tutapeleka magari hayo ikiwemo katika kata zenye uhitaji, ikiwemo Kata hii ya Nanjirinji ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali inatambua umuhimu, itanunua magari itayasambaza kote nchini na haitoacha kuleta katika kata ya Nanjirinji katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, katika haya magari 594, sisi katika Wilaya ya Chemba tuna upungufu mkubwa wa magari ya wagonjwa. Je, katika mgao unaokuja, Kituo cha Soya nacho kitapata mgao huo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Fatma Toufiq kwa swali lake linalolenga kuimarisha sekta ya afya msingi. Naomba kuendelea kumhakikishia kwamba, kama Serikali ilivyotangulia kutenga fedha na kununua magari 594 ya kubebea wagonjwa, ikiwemo na magari ya usimamizi wa huduma za afya na kuyasambaza kote nchini, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari haya na kuyasambaza kote nchini kwa kuzingatia kipaumbele kwenye maeneo yenye mahitaji makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika kituo cha afya alichokitaja cha Soya kilichopo Chemba, Serikali itafanya tathmini na kuona uhitaji na katika maeneo ya vipaumbele ya kupeleka magari haya ya wagonjwa pamoja na magari ya usimamizi wa huduma za afya, Serikali itazingatia uhitaji alioutaja katika kituo hiki na kuleta gari hilo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha afya msingi katika wilaya hii na katika Mkoa huu wa Dodoma.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 3

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Katika Wilaya ya Kilwa, tuna magari mengi chakavu ambayo yanahitaji ukarabati katika vituo vyetu vya afya na hospitali yetu ya wilaya. Je, ni lini Serikali italeta fedha kwa ajili ya ukarabati wa magari hayo ili kuboresha huduma ya magari ya wagonjwa katika wilaya yetu ya Kilwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Francis Ndulane kwa swali lake zuri linalolenga kuimarisha sekta ya afya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake, nichukue nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri wajibu wake wa msingi wa kusimamia utoaji wa huduma za msingi ikiwemo kwenye upande wa afya. Kwa kuwa Serikali Kuu tayari ilishanunua magari haya ya kutolea huduma ya kubeba wagonjwa pamoja na magari kwa ajili ya usimamizi wa huduma za afya na kuyasambaza kote nchini ikiwemo katika Wilaya ya Kilwa, sasa ni wajibu wa msingi wa halmashauri kupitia mapato ya ndani kuendelea kuyasimamia haya magari na kuhakikisha kwamba yapo katika mazingira mazuri, kwa kufanya ukarabati wa kila wakati kwa kadri inavyokuwa inatakiwa ili magari haya yaweze kutoa huduma za msingi kabisa kwa wananchi za kubeba wagonjwa, na huduma ya usimamizi wa huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, natoa maelekezo haya kwa mkurugenzi kupitia mapato ya ndani aweze kukarabati magari hayo ili yaweze kutoa huduma kwa wananchi.

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 4

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Katika Halmashauri ya Itigi nasi tulipata magari ambayo Serikali imetoa, lakini Kituo cha Afya Mitundu kipo mbali, tulipeleka Rungwa ambapo ni kilometa 194; na pale halmashauri tunahitaji gari kwa ajili ya kuhudumia hizi kata za karibu. Kituo cha Mitundu hakina gari kabisa. Je, Serikali ipo tayari sasa kutuletea na sisi gari katika kituo hiki ili wananchi wa Mitundu ambako kuna population kubwa na uhitaji ni mkubwa katika kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Waziri ametamka kwamba magari yatakuja?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Yahaya Massare kwa swali lake hili zuri linalolenga kuendelea kuimarisha sekta ya afya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotangulia kusema, kwamba Serikali imenunua magari 594 kwa ajili ya kubebea wagonjwa pamoja na usimamizi wa huduma za afya, magari haya yamesambazwa kote nchini, na ikiwemo pia katika halmashauri anayotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inaomba niendelee kumhakikishia kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inanunua magari mengine mengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kwamba bado kuna kuna kata na vituo vya kutolea huduma ya afya msingi ambavyo vina uhitaji wa magari haya. Serikali itanunua magari haya na kuyasambaza katika vituo hivyo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba yanaweza kutoa huduma za afya nzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaweka kipaumbele katika Kituo cha Afya cha Mitundu alichokitaja, na tutazingatia mahitaji aliyoyasema wakati wa kusambaza magari hayo mengine ambayo yatanunuliwa na Serikali.

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la kubeba wagonjwa katika Kituo cha Afya Nanjirinji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 5

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI alipotembelea Hirbadaw, aliahidi kwamba tutapata gari la wagonjwa. Je, Serikali ina mpango upi wa dharura ili tupate gari la wagonjwa, kwa sababu eneo hilo lipo mbali na makao makuu ya wilaya, na tumejenga Kituo kingine cha Basotu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kumpongeza Mheshimiwa Hhayuma Xaday kwa swali lake hili linalolenga kuimarisha sekta ya afya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ahadi ipo pale pale na Serikali itanunua magari kwa ajili ya kubebea wagonjwa, na vilevile itaendelea kununua magari kwa ajili ya kuimarisha sekta hii ya afya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa ahadi ipo pale pale. Tutakapopata magari haya, yatakaponunuliwa, yatasambazwa kote nchini kwenye uhitaji na tutazingatia ahadi ambayo ilitolewa na Mheshimiwa Waziri ya kuleta gari la wagonjwa katika jimbo lake Mheshimiwa Mbunge.