Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 294 2025-05-13

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza: -

Je, lini Serikali itawalipa watumishi wastaafu waliopandishwa madaraja kisha hatua hizo kusitishwa?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uwepo wa watumishi ambao walipandishwa vyeo na barua zao za kupandishwa vyeo kuingizwa kwenye Mfumo wa Taarifa za Utumishi na Mishahara na baadaye upandishwaji vyeo huo kusitishwa mwezi Juni, 2016 ili kupisha zoezi la uhakiki. Kundi hili linajumuisha pia watumishi waliostaafu kazi kabla ya Serikali kuruhusu tena upandishaji wa vyeo kuanzia mwezi Novemba, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia hatua hiyo, Serikali iliridhia na kuelekeza kuwa watumishi waliostaafu kwa aina hiyo, ambao wanastahili kulipwa madai ya malimbikizo ya mishahara ya kuanzia walivyopandishwa vyeo vyao hadi tarehe walipostaafu kazi, walipwe madai yao ya malimbikizo ya mishahara. Aidha, malipo ya madai haya yamekuwa yakifanywa na Serikali kwa wastaafu hawa kupitia kwa waliokuwa waajiri wao, nakushukuru.