Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 296 2025-05-13

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani wa kuunganisha gesi kwa ajili ya kupikia kwa Taasisi na nyumba za wananchi Mkoani Mtwara?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkoa wa Mtwara, Serikali imeshapeleka miundombinu ya usambazaji gesi asilia katika baadhi ya maeneo ambapo jumla ya nyumba 425 na taasisi nne zimeunganishwa na mtandao wa matumizi ya gesi asilia katika maeneo ya Mtwara Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, Serikali kupitia TPDC ipo katika mpango wa kuunganisha nyumba zaidi ya 865 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mtwara ambapo kuna miundombinu ya bomba la gesi, ahsante.