Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tunza Issa Malapo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuunganisha gesi kwa ajili ya kupikia kwa Taasisi na nyumba za wananchi Mkoani Mtwara?
Supplementary Question 1
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, nataka kujua, ni lini hizo nyumba 865 zitakuwa zimeunganishwa, kwa sababu wananchi wanahitaji huduma hiyo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa huduma ya gesi ya kuunganisha kwenye bomba ina gharama nafuu kuliko ya mitungi na kasi ya kuunganisha imekuwa ndogo sana. Nataka kujua, ni nini hasa mkakati wa Serikali wa kuongeza kasi ya kuunganisha ili nyumba nyingi zipate kuunganishwa wananchi wapate nafuu, hasa wale wenye kipato cha chini? Nakushukuru. (Makofi)
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri la kutaka kufahamu mipango ya Serikali ya kuhusiana na kuunganisha gesi asilia kwa wananchi wa Mtwara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa zile nyumba 865 mpaka sasa tumeshafanya usanifu wa kihandisi kwa ajili sasa ya kwenda kwenye hatua ya kuunganisha. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, muda wa hivi karibuni tutaanza zoezi hilo la kuunganisha kwa sababu tumeshafanya usanifu wa kiuhandisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili la mkakati wa Serikali, tayari Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu, aliekeza Wakala wetu wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha na wao wanaweka nguvu kwa kushirikiana na TPDC ili tuweze kuongeza kasi ya kuunganisha gesi asilia katika nyumba hizi zilizopo Mtwara pamoja na Lindi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali imeliona, tumeshaziambia taasisi zetu mbili, Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Maendeleo la Petroli wafanye kazi kwa pamoja ili washirikiane kuona kwamba kasi inaongezeka ya kuunganisha wananchi hawa wa Mtwara pamoja na Lindi vilevile. (Makofi)
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuunganisha gesi kwa ajili ya kupikia kwa Taasisi na nyumba za wananchi Mkoani Mtwara?
Supplementary Question 2
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nami naomba kuuliza, je, Serikali haioni iko haja sasa ya kuunganisha gesi ndani ya masoko yetu ya Stereo, Temeke, Keko na Mtoni kwa ajili ya baba lishe na mama lishe ambao wanapika ndani ya masoko hayo? (Makofi)
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao mkakati kupitia TPDC wa kuendeleza miradi ya kuunganisha gesi asilia kwa maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa masoko ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge, tumeyapokea, tutaenda kuyafanyia tathmini kuona lile ambalo linawezekana, ahsante. (Makofi)
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuunganisha gesi kwa ajili ya kupikia kwa Taasisi na nyumba za wananchi Mkoani Mtwara?
Supplementary Question 3
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, siku za hivi karibuni Wizara za Nishati walipita kugawa mitungi ya ruzuku na kiukweli kwenye maeneo ya vijijini kulingana na jiografia watu wachache sana walipata, je, Wizara ya Nishati, haioni haja ya kutumia ushauri huu kupeleka hiyo mitungi ya ruzuku na ikaweke kwenye Ofisi za Watendaji wa Kata ili kila mwananchi ambaye anataka kupata mtungi huo, aende na kitambulisho cha NIDA, afike ajiandikishe kwa wakati atakaopata, kuliko vile walivyokuwa wanafika kwenye eneo, watu wachache wanapata na baadhi ya vijiji wanakosa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inaonaje kuchukua wazo hilo ili hiyo mitungi ya ruzuku iwafikie Watanzania wote? (Makofi)
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwa ushauri wa Mheshimiwa Mbunge. Wakati tunaanza zoezi hili la ugawaji wa ruzuku ambapo tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa mkakati huu, ambapo tumeweza kupata mitungi takribani 420,000 ya ruzuku kwa ajili ya wananchi, na utaratibu tulionao ni kwamba kila mwananchi anayechukua mtungi ni lazima achukue kwa namba yake ya NIDA, ama kitambulisho chake cha NIDA. Kwa hiyo, kwa hilo tumezingatia kuhakikisha mwananchi mmoja anapata mtungi mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tulikuwa tumetenga mitungi takribani 3,255 katika Wilaya, na huu ndiyo mwanzo wa kuanza utekelezaji wa mkakati wetu wa nishati safi ya kupikia, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, mkakati huu ni wa miaka 10. Kwa mwaka huu wa fedha na kwa kipindi hiki tulikuwa tumetenga hii mitungi 420,000. Mkakati huu ni endelevu, tutaendelea kuja na mikakati na hatua mbalimbali za kuhakikisha tunaendelea kuwafikia wananchi wengi ili na wenyewe waanze kutumia nishati safi ya kupikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni mwanzo tu kazi inaendelea, kwa kipindi cha miaka 10 tutakuwa tumefikia 80% ambayo ndiyo maono ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved