Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 297 2025-05-13

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Nyimbili kuna minara miwili iliyojengwa kwa ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Mnara wa kwanza ni wa Kampuni ya Honora (Yas) ambayo ilikuwa TIGO na Mnara wa pili ni wa Kampuni ya Vodacom na minara hii yote imekamilika na inatoa huduma kikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Kata ya Ipunga na Isalalo bado hazijapata fursa ya kunufaika na miradi ya Serikali ya kuboresha huduma za Mawasiliano, hivyo kupitia UCSAF, Kata hizi zitafanyiwa tathmini ili kubaini changamoto za mawasiliano ya simu katika maeneo tajwa na kubaini mahitaji halisi na kuyaingiza katika zabuni zitakazotangazwa kulingana na upatikanaji wa fedha hususan katika mwaka wa fedha 2025/2026. (Makofi)